Thursday, 9 April 2015

Taifa stars ya Tanzania yajinasibu

Licha ya kupangwa katika kundi gumu na timu za Nigeria, Misri na Chad katika michuano ya kuwania kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon, kocha wa timu ya taifa ya Tanzani, Mdachi Mart Nooij amesema timu yake haiziogopi timu hizo.
Ameongeza kuwa badala yake, zitegemee pia upinzani mkali kutoka kwa Stars ambayo ana amini itakuwa imejiandaa vema kwa ajili ya mashindano hayo ambapo kushinda, kufungwa au kupata sare itakuwa ni sehemu ya matokeo.
Michuano ya Cosafa itakayofanyika nchini Afrika ya Kusini siku chache zijazo itakuwa ni sehemu ya maandalizi kwa Stars, kwa mujibu wa Nooij, ambaye anasema Stars itahitajika kutoa ushindani mkubwa.
kikosi cha Taifa stars
Taifa Stars itakuwa na kibarua kigumu katika kugombea nafasi mbili kwa ajili kwenda kucheza fainali.
Stars imeshuka katika viwango vya FIFA vya mwezi April vilivyotolewa Alhamis kutoka nafasi ya 100 mpaka nafasi ya 107 na kushuka huko kuna maanisha Nooij atalazimika kufanya kazi ya ziada kupenya katika tundu la sindano.
Licha ya kushuka nafasi nne katika viwango vya FIFA, Nigeria, sasa ikiwa nafasi ya 45 ni miongoni mwa timu ngumu barani Afrika zikiwa na historia ya kufuzu kucheza kombe la Mataifa ya Afrika na hata la Dunia, sambamba na Misri, ambayo imepanda nafasi 7 katika viwango hivyo na kuwa nafasi ya 51.
Katika kundi hilo, Chad ndiyo nchi/timu iliyo chini katika viwango hivyo, ikishuka nafasi 3 na kuwa nafasi ya 151.
Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) limetoa viwango vipya vya soka duniani huku Tanzania na Rwanda zikishuka kwa nchi za Afrika ya Mashariki wakati Kenya, Uganda na Burundi zikipanda viwango.
Kushuka na kupanda kwa viwango kunatokana na mechi za kirafiki za kimataifa za Fifa zilizofanyika mwezi Machi , ambazo matokeo yake ni sehemu ya kigezo.
Tanzania, baada ya kutoka droo ya 1-1 na timu ya Malawi katika moja ya mechi hizo za kirafiki, imeshuka kutoka nafasi ya 100 mpaka ya 107 huku Rwanda ikishuka nafasi 10 hadi ya 74 baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Zambia cha magoli 2-0 mwezi Machi.
Uganda ndio nchi inayoongoza katika Afrika ya Mashariki ikipanda nafasi mbili juu na kushika nafasi ya 72 baada ya kuwafunga Nigeria 1-0.
Burundi nayo imepanda kutoka nafasi ya 126 mpaka ya 123 mbali ya kutoka droo ya 2-2 na timu ya Mauritius.
Kenya pia imepanda nafasi moja juu na sasa ipo ya 117 huku ikiwa na rekodi ya kuifunga Shelisheli 2-0 katika mechi yake ya kirafiki.
Mbali na Afrika ya Mashariki, kiujumla kumekuwa na mabadiliko makubwa katika viwango hivyo vya mwezi April.
Miongoni mwa nchi zilizopanda ni Belgium ikiwa ya tatu baada ya kupanda juu nafasi moja kufuatia ushindi wake katika michuano ya Ulaya ya EUFA.
Brazil pia ni miongoni mwa nchi zilizopanda, ikiwa ya ya 5, ikipanda nafasi 1.
Nchi 10 bora katika viwango vya fifa ni
1. Ujerumani
2. Argentina
3. Belgium
4. Colombia
5. Brazil
6. Netherlands
7. Portugal
8. Uruguay
9. Swizerland
10. Uhispania

Jaji na wakili wapigwa risasi Italy

Jaji mmoja na wakili ni miongoni mwa watu waliouawa baada ya mshukiwa mmoja kuwafyatulia risasi ndani ya mahakama moja mjini Milan nchini Italia.
Maafisa wa idara ya mahakama wanasema kuwa mshukiwa aliyefyatua risasi ni mtu mmoja aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kutangazwa kufilisika.Mshukiwa huyo aliwapiga risasi watu wawili ndani ya mahakama kabla ya kumshambulia jaji ambaye angelisikiliza kesi yake ndani ya ofisi yake.
Mtu wa nne anaaminika kufariki kutokana na mshtuko wa moyo.Mshukiwa huyo alikamatwa kaskazini mwa Milan akitoroka kwa pikipiki.
Haijulikani jinsi mshukiwa huyo alivyoweza kuingia ndani ya mahakama hiyo huku akiwa na bunduki, kwa kuwa wageni wote hupitia vifaa vya kuwakagua ikiwa wana silaha.

Monday, 12 January 2015

Vijana waliokamatwa danguroni waachiwa Misri.



Mahakama nchini Misri, imewafutia mashitaka wanaume 26 waliokamatwa baada ya msako wa polisi katika jumba au danguro la wanaume na kjushitakiwa kwa kosa la kuchochea watu kutenda uovu.
Wanaume hao walikamatwa mwezi jana baada ya wanaume wengine 8 kufungwa jela kwa kosa la kuonekana kartika kanda ya video ambayo ilidaiwa kuonyesha ndoa ya wapenzi wa jinsia moja.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yamelaani serikali ya Misri, kwa ambavyo inawatendea wapenzi wa jinsia moja hasa kwa kuwafnayia uchunguzi katika sehemu zao za siri ili kubaini ikiwa ni wapenzi wa jinsia moaj au la.

Ingawa mapenzi ya jinsia moja hayajapigwa marufuku nchini Misri kwa wengi jambo hilo ni mwiko kwa jamii.
Familia za wale waliofutiwa mashitaka zilisherehekea sana mahakamani wakati jaji alipotangaza uamuzi wake.
Mwandishi wa Jarida la Daily Telegraph aliyeshuhudia kesi hizo, alisema kwamba kulingana na mwakaili, angalau mmoja wa wanaume hao alikuwa amebakwa wakati akiwa rumande.
Aliongeza kwamba washitakiwa walikuwa wamesimama kizimbani wakiwa wamefungwa mikono pamoja huku wakifunika nyuso zao.
Wakati wa kukamatwa kwao , viongozi wa mashitaka walisema kuwa mmiliki wa danguro hilo, alituhumiwa kwa kugeuza nyumba kuwa danguro au jumba na maovu.

Askofu akosoa Ulaya kuhusu Boko Haram.



Askofu mmoja nchini Nigeria ametoa wito kwa mataifa ya magharibi kufanya juhudi za kutosha dhidi ya Boko Haram kama ilivyofanywa dhidi ya washambuliaji wa kiisilamu nchini Ufaransa.
Askofu Ignatius Kaigama amesema mataifa ya magharibi yanapuuza sana tisho linalotokana na Boko Haram kwa watu wa Nigeria.
Askofu huyo wa Jos, aliongeza kwamba rasilimali zote zinatakiwa kutumika ili kuzuia juhudi za kundi hilo kukita mizizi nchini Nigeria. Pia amesema kwamba dunia inapaswa kuonyesha ari ya kutaka kuangamiza kundi hilo.
Kadhalika askofu huyo amesisitiza kwamba mauaji ya hivi karibuni ya mamia ya watu mjini Baga ni ishara kwamba jeshi la nchi hio limeshindwa kukabiliana na wapiganaji hao.

Onyo la askofu huyo linakuja siku mbili tu baada ya mashambulizi ya bomu kuwaua zaidi ya watu 20.
Mnamo Jumapili,washambuluaji wawili wa kike walifanya mashambulizi ya kujitoa mhanga na kuwaua watu wanne huku wnegine zaidi ya arobaini wakijeruhiwa mjini Potiskum
Siku moja kabla ya mashambulizi hayo, mashambuluaji mwingine w akujitoa mhanga alishambulia mji wa Maiduguri na kuwaua watu 19.
Mashambulizi haya yametokea baada ya taarifa kwamba mamia ya watu waliuawa wiki jana wakati Boko Haram ili poteka mji wa Baga katika jimbo la Borno.

Vita vipya dhidi ya waasi wa FDLR



Serikali ya Angola inasema kuwa uamuzi umechukuliwa na mataifa ya Afrika kuingilia kijeshi harakati za waasi wa kihutu kutenda uhalifu Mashariki mwa Congo.

Afisaa mmoja mkuu (Joaquim do Espirito Santo) anasema kuwa mkutano wa kikanda uliotarajiwa kufanyika leo, umefutiliwa mbali kwa sababu ya hofu ya kuchelewesha mipango ya kijeshi dhidi ya waasi hao.

Umoja wa mataifa ulithibitisha mwishoni mwa wiki jana kwamba waasi wa FDLR wamepitwa na muda waliowekewa wa mwisho kwao kusalimisha silaha.


Wiki jana Rais wa DRC, Joseph Kabila, aliambia katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kuwa jeshi la nchi yake liko tayari kupambana na waasi hao.
Mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Mataifa, (Martin Kobler) amesema kuwa hatua za kijeshi ndizo pekee zinahitajika kuchukuliwa dhidi ya waasi hao kwa sasa.

Sunday, 11 January 2015

Afisa wa kanisa apigwa risasi mombasa.


Polisi nchini kenya wamesema afisa mmoja wa kanisa nchini kenya apigwa risasi na kuuawa hapohapo alipokuwa akielekea kanisani kufanya maombi.
Madhumuni ya mauaji hayo bado hayajajulikana lakini muungano wa makanisa mjini mombasa yamesema kuwa haya yatakuwa ni mauaji ya kidini.
Mauaji ya afisa wa kanisa hilo yanatishia wakaazi wa mombasa waliouanza mwaka kwa amani baada ya machafuko mengi ya mwaka 2014.
Polisi wamesema afisa huyo alipigwa risasi wakati alipokuwa anaenda katika shule moja mjini mombasa kwa ajili ya kufanya maombi.
Mkuu wa upelelezi na uhalifu mjini humo aliejulikana kama 'Ondiek' amesema mtu mmoja aliekuwa na bunduki alifatulia risasi afisa huyo na kufa hapohapo.
Ondiek amesema kuwa polisi kwa wakati huo walikuwa wameshikilia doria shuleni ghafra walisikia sauti za risasi na walipo mfatilia alikimbia katika vitongoji vya kalibu na shule hiyo na kupotea....